ASAKWA NA KUTISHIWA KUUAWA NA WAISLAMU SABABU YA MASHARUBU YAKE...

Malik Amir Mohammad Khan Afridi.
Baba mmoja wa Pakistani ameelezea jinsi anavyokabiliana na vitisho vya kuuawa na amekuwa akikimbilia mafichoni - sababu ya masharubu yake yenye urefu wa inchi 30.

Waislamu wenye msimamo mkali wamegadhibishwa mno na ndevu za Malik Amir Mohammad Khan Afridi kiasi cha kumteka nyara mfanyabiashara huyo na kumshikilia kwenye pango kwa mwezi mmoja hadi hapo zitakapokuwa zimenyolewa.
Lakini licha ya migongano yake na wanajeshi kuhusiana na sharafa zake alizotunukiwa - zinazosemekana kuonesha urijali na neema - baba huyo wa watoto kumi, kutoka Peshawar, Pakistani, sasa amezikuza, akiasa kamwe hatodhalilishwa na wahuni hao tena.
Afridi alisema: "Sipendi kuvuta sigara. Mimi si mpenda ugoro, au kunywa. Hili ni chaguo langu pekee katika maisha yangu. Sijawahi kutoa kafara chakula, lakini masharubu. Ni maisha yangu. Si sehemu ya maisha yangu, Ni maisha yangu.
"Watu wananipa heshima kubwa mno. Ni utambulisho wangu."
Masharubu hayo imekuwa mapenzi makali ya Afridi tangu alipoanza kuzifuga akiwa na umri wa miaka 22.
Sasa anatumia dakika 30 kwa siku kupunguza masharubu yake hayo. Gharama ya mafuta ya nazi na sabuni vinavyotumika kutunzia hugharimu Pauni 100 kwa mwezi.
Licha ya gharama hizo, vitisho hivyo vya kuuawa, hofu ya kushambuliwa na kutumia vipindi virefu mbali na familia yake, vyote vinamwandama, anasisitiza.
"Najisikia furaha. Itapokuwa kawaida, hakuna atakayenifuatilia. Nimeshazoea kufuatiliwa kote huko na ninapenda mno."
Lakini Afridi amekuwa makini mno na wanamgambo wa kundi la Lashkar-e-Islam, ambalo linadhibiti vitongoji vya wilaya ya Kyber nchini Pakistani, karibu na mpaka na Afghanistan.
Kundi hilo lilikuwa likijaribu kushurutisha amri kali kwamba masharubu na ndevu lazima zinyolewe au zipunguzwe ziwe fupi.
Alipokataa kulipa fedha za ulinzi kwa kundi hilo, alitupwa kifungoni kwenye pango hadi atakapokuwa amenyoa.
Akiwa amenusurika maisha yake, Afridi alianza kuyafuga tena masharubu yake kwa kile alichofikiri kilikuwa kikiendana na mji salama wa peponi wa Peshawar. Lakini alianza tena kupokea vitisho mwaka jana.
Kwa sasa amelazimishwa kuiacha familia yake kwa vipindi virefu na kuhamia kusini mwa Faisalabad ambako anajihisi yuko salama.
Afridi anaamini masharubu yake yanaweza kuwa tiketi kwake na familia yake kuepuka usumbufu.
Alieleza: "Nataka kuishi, ndio maana nataka kuondoka Pakistani.
"Chaguo langu la kwanza litakuwa nchi ya Kiislamu kama Dubai.
"Lakini pia natakusudia kwenda katika nchi kama Marekani, Canada au Uingereza. Napenda kuiomba serikali ya Uingereza inisaidie."

No comments: